Monday, May 31, 2010


Huyu ndiye mwana na mjanja asiyepitiliza anayemiliki blog hili la kitaa kwa ufahamu zaidi. Anaitwa Emmanuel E. Mnzava au ukiwa na pumzi za kutosha sema Mzeiya wa milazo "wamilazo". Mchizi ni mtangazaji wa radio moshi fm pande za kilimanjaro na anasukuma dambwe kama The base, Mid-Morning Cruz,Supreme Countdown,Project 120 na dabwe nyingine kibao na pia anamwaga material katika chuo yani pande fulani kati hivi ya coarse ya Broadcasting and Journalism Radio and Tv Production.

PISHI LIMEWIVA

Mambo vipi Mtanzania!!!



Kama upo poa,furaha ndio inatawala zaidi katika moyo wangu. Binafsi nipo safi ndio mana leo nataka nikupe kinaga ubwaga kuhusu blog hili la kitaa kwa ufahamu zaidi.



Blog hii ni ya kitaa kwa ufahamu zaidi litakujuza mambo mengi ya kisiasa,kijamii,kiuchumi na burudani bila kusahau kuwa mungu daima tunamueka mbele namaanisha maswala ya dini yatakuwepo.



Kiukweli mchakato umeanza rasmi kwa mwendo wa gari,ndege,pikipiki,baiskeli au ukianza kutembea, unaanza taratibu kisha unachukua kasi ya ajabu kwa wewe upendavyo.



Kila jambo kwa kulifanya kwa umakini unahitaji kutafakari,kuchambua mambo na kuliwakilisha kwa umakini ila lazima upate mawazo kutoka kwa wengine maana hakuna aliyekamilika.



Nashukuru kwa kufahamu haya machache!!!



Kaa tayari wewe mkubwa,wakati na mtoto.



Bidae!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Saturday, May 29, 2010

BE READY

Mambo vipi mtanzania wa kweli,naamini poa karibu sana pande hizi za kitaa cha kuahabarishana,kufahamishana na kuburudishana. Hii ni blog ya home ambayo itakujuza mengi kuhusiana na mambo mbalimbali.

Kiukweli kaa tayari na pia unayo nafasi ya kutoa maoni yako nini hasa unakihitaji.