Friday, October 8, 2010

BANGI, NIBANGUE MPAKA CHEEEEEEEEEEE!!!!

Bangi ni nini?

Kwa hapa nchini na baadhi ya nchi, bangi imetambulika kama dawa ya kulevya ambayo imekuwa na majina mengi kutokana na kutumiwa na kundi la vijana zaidi kuliko watu wazima.

Bangi imekuwa ikijulikana kwa majina mengi ikiwamo, dawa, ganja, hashish, kijiti, marijuana, kaya blunt na mengineyo, ilimradi kutegemeana na sehemu inapotoka.

Watumiaji wengi wamekuwa wakiitumia kwa kuvuta kama sigara au wengine hutumia kwenye kiko kwa kuvuta.

Bangi ni bidhaa iliyochanganyika na kemikali hatari ambazo ni sumu na huathiri afya.

Wapo baadhi ya watumiaji wa bangi ambao wamekuwa wakiitumia kwa kuiweka katika maji wakiifanya kama majani ya chai na wengine huchanganya kwenye chakula.

Athari ya bangi ni ipi?

Wanasayansi wamebaini kuwa matatizo makubwa yanaanza kupatikana kutokana na bangi kuingia kwenye ubongo wa mtumiaji na huathiri mfumo mzima wa akili.

Tatizo kubwa linalomkumba mvuta bangi ni kunyemelewa na magonjwa ya ugonjwa wa shinikizo la damu (BP), kupoteza kumbukumbu, mawazo, anaridhika hata kama ana matatizo.

Pia mtumiaji wa kila siku anakuwa akikumbwa na mabadiliko ya mara kwa mara katika ubongo wake.

Imebainika kuwa bangi inachangia kuongeza mapigo ya moyo kutoka asilimia 20 hadi 100, muda mfupi tu wa saa tatu baada ya kuvuta.

Bangi huaribu mapafu, kwani ina zaidi ya asilimia 50–70 ya kemikali aina ya carcinogenic hydrocarbons kuliko mvutaji wa tumbaku.

Mtumiaji wa bangi hupumua kwa tabu sana kuliko yule anayevuta tumbaku ingawa wote wanaharibu mapafu, pamoja na kuwa na uwezekano mkubwa wa kukaribisha ugonjwa wa kansa.

Imebainika kuwa watu wanaovuta bangi wamekuwa wakisumbuliwa zaidi na matatizo mengi ya kiafya.





Tafiti za wanasayansi

Kumekuwepo kwa baadhi ya tafiti zilizokuwa zikiruhusu uvutaji wa bangi kwa madai kwamba ilisaidia wagonjwa waliosumbuliwa na msongo wa mawazo, hali hiyo imesababisha baadhi ya nchi kuruhusu matumizi yake.

Pamoja na mawazo ya wengi kufikiria kuwa kutokana na nchi ya Jamaica ndiyo ilikuwa mstari wa mbele kwa watumiaji wengi ingekuwa ya kwanza kuruhusu bangi, lakini ukweli ni kwamba nchi ya Canada ndiyo ilikuwa ya kwanza kukubali bangi kutumiwa kama dawa ya maradhi.

Baada ya utafiti huo wa awali hivi karibuni watafiti wengine wamegundua kuwa matumizi ya bangi kwa muda mrefu yanasababisha kujiongezea madhara badala ya kutibu kama ilivyokuwa ikisemekana hapo awali.

Watafiti hao wamekwenda kinyume na wale wa kwanza kwa kusema kuwa matumizi yake yana uwezekano mkubwa wa kumletea mtumiaji magonjwa ya kupungua uzito mara kwa mara, magonjwa ya figo, ini na ugonjwa wa akili.

Watafiti waliogundua athari hizo ni wale wanaotokea nchini Australia ambao katika utafiti wao wamegundua kuwa zaidi ya vijana 3,100 walio katika umri wa miaka 20 ndio wamekuwa watumiaji wakubwa wa bangi.

Utafiti wao umekwenda mbali na kubaini kwamba asilimia 18 ya vijana hao ni wale waliojiingiza katika matumizi ya dawa hizo za kulevya kwa muda wa miaka miwili au mitatu.

Asilimia nyingine 16 ya vijana wa umri huo wamebainika kutumia kwa muda wa kati ya miaka minne hadi mitano.

65 kati ya watumiaji wamegundulika wameshaathirika na maradhi ya ugonjwa wa akili.

Wakati hao wakisumbuliwa na tatizo hilo wengine 233 wamebainika kuathirika kwa figo na ini.

Watafiti wamebaini vijana wengine kati yao wanasumbuliwa na tatizo la kupata uchizi (wehu).

Baada ya kubaini hayo watafiti wametoa ushauri kwa vijana kutotumia dawa hizo za kulevya kwa vijana kwa zaidi ya miaka sita au zaidi tangu pale siku ya kwanza alipoanza kutumia.
Wanasema kuwa kwa wale ambao sasa wamevuta kwa muda mrefu kati ya miaka 15 na zaidi wengi wao wamekumbwa na tatizo la kiakili.

UTANIPA MAJIBU JUU YA HILI KAMA UTAFEEL.

KWA MAONI, MAWAZO JUU YA BLOG HII NA CHOCHOTE UTAKACHOSOMA PLEASE MDAU NITONYE KUPITIA BARUA PEPE ( E-MAIL) HIYO HAPO JUU.

Friday, October 1, 2010

MAMBO VIPI WAUNGWANA MPO POA???

LONG TIME MBAYA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Me mzima wa afya na naendelea poa na kuchaplika hapa town. Ubize ulikuwa kiasi lakini si sana kiivyo kwani yapo mazuria ambayo nimekuandalia ya kuyafahamu na kujiuliza ili tuweza kusongesha gurudumu la maisha.

Ndani ya mjengo wa MOSHI FM kama kawa kama dawa mambo nayasongeshwa kwa sana tu, na kama upo kanda ya kaskazini ( Tanga,Manyara,Kilimanjaro na Arusha) unatusoma kwa 90.2. Pindi nazishona zile zile Mid-Morning Cruise jumatatu hadi ijumaa saa 2.00-5:00 asubuhi, The base kila jumatatu - alhamisi saa 7:00-10:00 mchana, Project 120 kila ijumaa saa 7:00-10:00 mchana, Nipe Nikupe kila jumamosi na jumapili saa 1:oo-4:00 asubuhi na Supreme countdown jumamosi saa 12:00-02:00 usiku.


Kama kawaida pia nakandamiza kama ticha wa masomo ya uandishi na utangazaji katika chuo kikongwe na maarufu cha udzungwa. Karibu ujiunge.

Mwana nimerudi kwa kishindo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Sunday, July 18, 2010

CHEKI SWAGGAZ ZA PROJECT 120!!!!!!!!!!!!

HOT PINDI NDANI YA MOSHI FM 90.2

Hii ni shoo kali ndani ya redio moshi fm kila ijumaa saa 7 hadi saa 10 jioni, wengi hawakosi kuisikiliza sikjui wewe. The big host wa hot pindi hili ni Mzeiiyaaaa wa milazo. Mzazi usijaribu kusikiliza hutaacha.


Nyie watoto kwa makamuzi si mchezo mnafanya balalaaaa. Huyu ni Ntoly Mayombole baada ya mzuka aliamua kuvamia shoo kwa upande wa pili wa studio.




Hisia za mziki zinapogusa mahala penyewe hakuna mkubwa wala mtoto, bosi wala mfanyakazi na milazo tata ni raha raha raha mpaka mwisho mwisho!!!!!!!!!!. Mwenye shati la drafti nyekundu na nyeupe ni Meneja wa redio moshi fm, Bw Deus Mworia.




Mwenye Tshirt ya mistari ya bluu na nyeupe(kushoto) ni Dj Poggo na mwenye tshirt nyekundu (kulia) ni Dj Q. Machizi ambao wanawakilisha vema katika shoo hii kali pia wagonga pini ndani ya club laliga


Mwenyewe headphone ni host wa hot pindi la project 120 Mzeiyaaa wa milazo na kwa mabli ni madj's wakigonga pini kwa ushirikiano.


The host wa hot pindi "project 120" Mzeiiiyaaaaaaaa akichongana na Dj Poggo.

Usiache kusikiliza Moshi Fm kwa vipindi vikali baada ya marekebisho ya nguvu.








HAPPY BIRTHDAY MADIBA!!!!!!!!!

HONGERA MANDELA MUNGU AKUZIDISHIE UMRI

Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela leo anatimiza miaka 92, huku ulimwengu ukisherehekea kwa mara ya kwanza, "Siku ya Nelson Mandela Duniani" kwa heshima ya kiongozi huyo.


Viongozi wa kimataifa na watu wa kawaida nchini Afrika Kusini na nje ya nchi hiyo, wameahidi kujitolea kuhudumia jamii kwa dakika 67 katika ishara za kuadhimisha miaka 67 ya kiongozi huyo kushughulikia kisiasa.
Tangu kuondoka madarakani, Mandela amejitokeza hadharani mara chache tu. Juma lililopita alikwenda kwenye uwanja wa michezo wa Soccer City mjini Johannesburg, kuwapungia mkono mashabiki wa kandanda kabla ya kufunguliwa mchezo wa fainali wa Kombe la Dunia, lakini hakubakia kutazama mchezo kwa sababu ya hali yake dhaifu ya afya.

Tuesday, June 22, 2010

AFRIKA BYE BYEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Wenyeji wa kombe la dunia, Afrika Kusini wametupwa nje ya fainali za kombe la dunia pamoja na kwamba walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ufaransa katika mechi yao ya mwisho.
Hata hivyo Vigogo wa ulaya Ufaransa wameliaga kombe la dunia wakishika mkia kwenye kundi baada ya Afrika Kusini kuwabebesha virago.
Wawakilishi wengine wa Afrika, Nigeria watabidi wajilaumu wenyewe kwa kuliaga mapema kombe la dunia, kutokana na nafasi nyingi za wazi walizozipoteza.
Nigeria ilihitaji ushindi kwenye mechi yake dhidi ya Korea Kusini, lakini iliambulia sare ya magoli 2-2, yalifungwa na Kalu Uche kwenye dakika ya 12 na Yakubu kwa njia ya penalti kwenye dakika ya 69.
Matumaini ya Afrika yamebaki kwa timu za Algeria, Ghana na Ivory Coast.

Monday, June 21, 2010

CAMEROON BYE BYEEEEEEE!!

Cameroon timu ambayo ilikuwa miongoni mwa timu zilizokuwa zikitajwa kama “tumaini la Afrika”,imeyaaga mashindano hayo baada ya kufungwa jumla ya magoli 2-1 na Denimark


Timu hiyo imebakiza mechi moja kwa heshima ya michezo ingawa kushinda si sababu ya kuendelea bali kujiwekea sifa nzuri kiduchu ila kufungwa ni aibu ambayo itakuwa na historia kwa timu hiyo kubwa.

Mchezaji mkali Eto alisadikika ni kati ya wachezaji ambao watacheka na nyavu ingawa amecheka na nyavu mara moja.

Poleeeeni ndio michezo.!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1

RAIS KIKWETW ACHUKUA FOMU YA URAIS

Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya M. Kikwete, Leo mchana amechukua fomu ya kutetea kiti chake cha uraisi kupitia chama cha mapinduzi huko mkoani dodoma.

Kikwete anakuwa mwanachama wa kwanza kuchukua fomu za kuwania kiti cha uraisi, uchaguzi utakaofanyika oktoba mwaka huu.

Akikabidhiwa fomu na Katibu mkuu wa chama hicho Yusuph Makamba, kuliambatana na sherehe za kumpongeza huku wana CCM wakijitokeza kwa ajili ya kumdhamini.


Kikwete akikabidhiwa fumu na Makamba!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Saturday, June 19, 2010

WEEKEND NJEMA WAUNGWANA!!!!


USAFIRI UPO MWAKE MBAYA

Kila mtu hapa duniani anapenda kuishi vizuri ila wote tungekuwa matajiri au uwezo sijui nini ingetokea au wote tungekuwa maskini sijui nini kingetokea. Wenzetu wa magaharibi wamepiga hatua kiteknologia sasa sisi wakinakabwela mmmmmmhh!!!!!

Yani ukiupata huu usafiri kwa hapa tanzania kila mtu mimacho kodooooooooooooo mwanzo mwisho.


a.k.a fuvu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

DHAHABU YA KASKAZINI

Kila kukicha tunategemea kuona mziki wa Tanzania unawanufaisha wasanii wa kitanzania na kufika nlevel za kimataifa kwa lengo la kujulikana huku wasanii wanachipikua tukitegemea pia kufanya vizuri.

Kanda ya kaskazini ni moja kati ya kanda zenye wasanii wazuri Tanzania, lakini kilio chao ni kukosa air tym haswa kwa redio za Dar na kutoaminiwa kwa studio za mikoani kuwa zinafanya vizuri huku wasanii hawa wakipata changamoto ya kukosa ushirikiano baina yao.



Suleiman Zitueni “Top B” a.k.a Dhahabu ya kaskazini ni mmoja kati ya wasanii wanaofanya vizuri kanda ya kaskazini ila si msanii mchanga wa la wa juu bali wa kati anyefahamika katika mziki wa kizazi kipya.

Kila mtu anayo hatua ya maisha kama alivyo msanii huyu akielezea hatua ya aliyopiga mpaka alipofikia katika mziki huu wa kizazi kipya.

Top B anasema alianza mziki mwaka 2005 ndani ya mkoa wa Kilimanjaro,moshi mjini kama msanii wa kujitegemea na jina hili alipewa na mama yake.

“Top B lina maaana ya Top in bongo fleva na jina hili nilipewa na mama yangu baada ya kutiririka ma freestyle kila kukicha ndio akaniambia hakika mwanangu utakuwa top katika mziki huu” alisema Top B

Anasema rekodi ya kwanza katika game ilikuwa inaitwa Kifaa, kazi ilishonwa 360 production kwa produza Wise Mad studio toka pande za huku ingawa ngoma hii haikupata air time ya kutosha.

Ngoma hii ndio ilianza kumtambulisha na kuanza kujulikana katika ukanda wa kaskazini ingawa redio zilikuwa mbili Kibo Fm na Kili Fm ila ngoma ikaendele kugongwa kiaina.

Baada ya safari hii ya kutambulika, Top B anasema alipata nafasi ya kujiunga na kundi la mzizini camp, kundi lilokuwa na nguvu kipidi hicho baada Meneja wa kundi hilo Bw. Kalage kumuita.
“Meneja baada ya kunisikia aliniomba nijiunge na kundi hilo na alinichagua kuwa kiongozi na washkaji tuliokuwa nao ni Rhymes B,Ommy, Bilo one na Kupa.” Alisema Top B



Baada ya wiki moja tuliondoka kwenda Dsm kufanya album ya kundi katika studio za Metro studio chini ya mkono wa Allan Mapigo na Big tyme kwa Comoriel na kufanya rekodi sita kama watanzania ya Rhymes, Rudi mpenzi ya kupa,wachakusita ya Bilo one na nyingine.

“Ukweli mimi sikufanya ngoma hata moja zaidi ya kujazia sauti yaaani vile viitikio (back vocal) ila ngoma moja ya Rhymes B inaitwa sikiliza nilipata nafasi kidogo kuweka viji mistari kidogo maana nilifika wiki moja tukaenda dsm wakiwa tayari wameshajiandaa” alisema Top B.

Baada ya kurudi Mji wa wagumu “Moshi” tukasikiliza ngoma tulizofanya, wakasikiliza ngoma inaitwa “sikiliza” ambayo nilipata shavu nene kidogo na niligonga na Rhmes B, nikawa nimefanya poa,ikabidi turudi Dsm kwa Comoriel na kuirudi na nikapata verse.

Ujio kutoka bongo kwa mara nyingine, walisikia studio ya MO-TOWN RECORDS na kupanga kuitembelea ili kujua kazi zinavyokwenda ila siku hiyo Top B anasema hakwenda kwa ajili ya majukumu ya home.

Ndani ya MO-TOWN RECORD walikutana na produza Tripple A na kuwapa ofa ya ngoma moja bure na kuanza kazi ya kugonga beat tyme hiyo.

“Machizi baada ya kupata ofa walinicallm, nikatimba na nilikuwa na ngoma yangu iliyoitwa usiondoke, tukagonga beat then tukarudi skani kwa ajili ya kupangana katika verse” Alinitonya Dhahabu ya kaskazini.

Walijipanga kama kundi la watu wanne na kushambulia ngoma hiyo ya kwanza katika kundi ingawa wapo watu hawakusikika katika ngoma hii ya usiondoke.

“ Sijui sababu ni nini…..Meneja aliwatoa Kupa na Ommy katika ngoma hii na Bilo One aliyekuwa Dsm alikuja na kufanya vocal, so tulirudia tena ile ngoma kwa mara ya pili” Alisema Top B.

“ Produza alituahidi baada ya muda mchache tutaipa, nakweli ikawa hivyo na kuipeleka redio na ni kati ya ngoma kali zilizotesa kanda ya kaskazini na kundi la mzizini kujulikana baada ya kuachiwa nikiwa nashika verse ya kwanza na chorus” alinena Top B
.


Mchizi alijulikana na kupata makubaliano ya kuwa chini ya studio ya MO-TOWN RECORDS kwa ajili ya kufanya album.

“Nilitamani sana kufanya kazi zangu mwenyewe, so nilifurahi na kukubali makubaliano hayo na nikarudia ile nyimbo ya kifaa” Alisema Top B.

Akazidi kumwaga mavocal katika studio hiyo na kugonga UNAJUA akimshirikisha Voice wonder, ZEINA alisimama mwenyewe, RIZIKI POPOTE akimpa shavu Ras Lion na NAKUTHAMINI akigonga na Muddy best.

Baadhi ya ngoma zilipata air time yakutosha na kumtambulisha na kuwa msanii wa kati ambaye anafahamika na baadhi ya watu Tanzania huku ukanda wa kaskazini akiuteka zaidi.

“Nilipata support kwenye baadhi ya redio ila ngoma ya mwisho ya NAKUTAHAMINI haijapata air tym kwa redio za nje ya kanda ya kaskazini na nilipata nafasi ya kufanya video ya UNAJUA pale Empty soulz kwa Osama, video ambayo ndio ilifanya nijulikane na watu wanaonikubali” alisema Top B.

Kwa sasa Msanii huyu amekuwa kimya baada ya kuachia ngoma yake mwezi wa kwanza mwishoni ila maandalizi ya album yapo jikoni huku akitafakari jina la album hiyo.

“ Nategemea kumaliza album yangu, niitangaze ili kwenda sokoni kama ahadi yangu kwa mashabiki wangu na sitaishia hapa ila niwe msanii wa kimataifa na mwenye kujali sanaa ya mziki”

“ Watanzania nawashauri watoe sapoti kwa wasanii na mziki wa bongo fleva na pia wasanii wawe makini kwenye kazi yao isipuuzwe, Nawapenda wote, saaaana saaaana” Alimalizia kwa kusema hayo Top B.

Hii ni hatua ya msanii huyu wa mziki wa kizazi kipya katika mziki wa kizazi kipya na nitakuwa nakufahamisha wasanii wanaofanya vizuri haswa wale wachanga.

Ni hayo tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Friday, June 18, 2010

NYUMBANI NI NYUMBANI

Ukweli ni mzuri maana ni moja kati ya mambo yanayokufanya ufanikiwe. Me mtoto wa kipare kutoka Vudee, pande za same juu.

Siku chache wiki hii nilikuwa kimya na nilitembea pande za home, najivunia sana ingawa ni mara ya kwanza kwa pande nilizokwenda na niliona vitu ambavyo sijaweahi kufikiri kama vipo huko.

Napata wasiwasi labda wengine hawafahamu ila napata raha kwa vivutio vilivyopo pande hizo za same juu.



Unaweza kufikiri hapa ni ulaya laaaaaa!. ni same juu akita mlima ya shengena hapo katikati si maji nimawingu yakiwa yametulia


Kuna barabara zinazozunguka mlima huu wa shengena na kwenda kwenye vijiji vingine ila hapo tuliogopa kushuka kwani kunatisha.


Kuna miti ya ajabu sanaa ambayo na hisi ni mizuri.


Ilikuwa safari ya siku moja tu ingawa ilikuwa tamu na ngumu. Tulipofika maeneo ya tambaraer na njaa ikiwa kali tuliamua kujipoza kwa picha. Huyu ni rafiki yangu Mustafa Ngetwa.


Dereva tuliyekuwa naye, Hassan.


Ilinibidi nitafute japo ndizi ila picha za kustukiza si nzuri jamanii!
Toka pade hizooooooooooo............................................!!!!!!!!!!!!!!!!!!.



MTOKO WA BENJAMINI WA MAMBO JAMBO

Msanii wa Miondoko ya Ragga Benjamin wa Mambo Jambo anatarajia kutoa track yake mpya mwanzoni mwa mwezi wa saba akimpa shavu saigon ingawa hakuitaja jina.


Kazi amifanya ndani ya mzuka rekodi, produza akiwa yeye mwenyewe kama alivyoishona nimefulia.

Benjamin amewaambia mashabiki wake wakae tayari kuipokea track yake mpya kwa sababu ni kali zaidi ya nimefulia na mashabiki wakae tayari kwa album yake mpya ambayo baadhi ya track zimekamuliwa na producer Miikka Mwamba kutoka nchini Finland na Baadi ya track amefanya yeye mwenyewe.

ZAMU KWA ZAMU NDANI YA TMK WANAUME FAMILY

Jibaa wa wanaume out!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Siku chache baada ya kundi la TMK Wanaume kuwasababishia mtoko Chegge pamoja na Mh.Temba...hatimae imefika zamu ya kichwa cha mzee mzima"KR".



Jibaba 'KR' amewaka wazi kuwa wakati wowote wiki hii atarelease wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la 'MAPEMA'.

Amesema pini hilo amelifanyia studio za Fishcrab chini ya Producer bwana mdogo Lamar...huku ndani yake akiwa amempa shavu mzee wa malavidavi namzungumzia Cassim Mganga kutoka familia ya TipTop kutoka Manzese.

Sikiliza Moshi Fm, kwenye show ya the base kila jumatatu hadi alhamisi na ijumaa ni project 120 kuanzia saa 8 hadi saa 10. Hapa utawasoma maswahiba waukweli, Mazimu, Dj clever na Mzeiya wa milazo.

Yeaaaaaaah..................

CHIDI NA MZEE YUSUPH SERO MOJA

Ngoma itambae ili Alamba tenaa aaaammh!!!!!!!!!!!!!!

Nyepesi ni kwamba mzigo ambao kila mmoja atakuwa nahamu ya kuusikiliza naongelea kolabo ya ajabu kuwahi kusikika kati ya msanii bora wa hiphop kwa 4 years mfululizo CHIDI BEENZ na MZEE YUSUPH! hahaaaa,alambaa tena aaaamh. Mpaka sasa bado jina la ngoma hiyo halijapatiakana. So tulisubirie


Chidi Benzi a.k.a Kin Kong akiwa live kwenye michano na amevaa moja kati ya Tshirt ambazo zilitoka kwa ajili ya kumkumbuka TID baada ya kusukumwa lupango.


Mzee Yusuph akionyesha jinsi ya kuceza kwa hisia. Jamaaa ambaye anafanya poa sana katika mziki wa taarabu na amukuwa mchukuaji sana wa tuzo nyingi za KILI.
Oya tusubirie hilo pini la mkali wa hip hop na mkali wa taarabu.

Thursday, June 17, 2010

Monday, June 14, 2010

WEKA ASILIMIA ZAKO

Haya ndio maisha ya mapenzi.

Katika maisha ya mapenzi kuna mambo mengi ambayo unakutana nayo endapo unaye mpenzi au upo kwenye ndoa au umeamua kuishi na yule ambaye anakufaa. Hebu jaribu kutafakari katika maisha ya sasa haya;

Fumanizi
Mauzo ya condom
Waliozini
Matukio wakati wa mapenzi mfano kuvunjika kitanda
Waliopata wapenzi wapya
Waliyoachwa(kugombana na kuachana) yaaani Ndoa zilivunjika

Wanaoshinda nyumbani na familia zao
Mahudhurio ya gesti
Wangapi wanatumia neno I LOVE YOU.

Nahisi utakuwa umenisikia vizuri, jaribu kutafakari katika maisha ya sasa jambo gani ambalo linatiafora au kushamiri katika maisha ya mapenzi na unalipa asilimia ngapi na kama umesikia vizuri jaribu kuyapanga kiasilimia au la kwanza hadi la mwisho.


Nangojea majibu yako.

UJERUMANI YACHINJA KOMBE LA DUNIA

Ujerumani 4-0 Australi

Kikosi cha kocha Joachim Löw kimedhihirisha umariri wake wa kusakata ngozi ya"Jabulani" kwa ustadi mkubwa baada ya kushinda mechi yake ya kwanza kwa kuichabanga Australia mabao manne kwa bila.

Washambuliaji, Lukas Podolski na Miroslav Klose waliliona lango la Australia katika dakika 30 za kwanza. Magoli mawili ya Ujerumani yaliongezwa katika kipindi cha pili cha mchezo, na Thomas Müller na Cacau.


Hata hivyo katika kipindi cha pili Australia ilibakiwa na wachezaji 10 baada ya Tim Cahill kuonyeshwa kadi nyekundu kwa sababu ya kucheza faulo.

Hapo awali Ghana iliibwaga Serbia kwa bao moja la penalti baada mchezaji wa Serbia kuunawa mpira ndani ya eneo nyeti katika dakika ya 86.

Kabla ya mechi hiyo Slovenia ijipatia ushindi wa kwanza katika mshindano ya kombe la dunia kwa kuifunga Algeria bao moja kwa bila.

Tunaendelea kucheki michuano ya kombe la dunia ila kwa matokeo na vibwanga vingine ni hapahapa katika blog ya kitaa kwa ufahamu zaidi.

Vijana Vyuo Vikuu Dodoma Waandamana kumuunga mkono Rais Kikwete kugombea Urais kwa tiketi ya CCM Mwaka huu!!

Mwenyekiti wa CCM taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewaongoza wanachama wapya wa CCM kula kiapo cha utii kwa Chama Cha Mapinduzi muda mfupi baada ya kuwakabidhi kadi za uanachama wakati wa maandamano ya kumuunga mkono yaliyofanyika mjini Dodoma.


Baadhi ya vijana kutoka vyuo vikuu mbalimbali mjini Dodoma wakiandamana kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuchukua fomku kwaajili ya kugombea nafasi ya urais 2010.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika vyuo vikuu mbalimbali mjini Dodoma walishiriki katika maandamano ya kumuunga mkono kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi ya Urais mwaka huu kwa tiketi ya CCM.

Vijana wengine mpo wapi na vyama vyenu au hamuwapendi viongozi wenu wa taifa?

SWAGGA YA THE NGOSHA



Fid Q: So Swagtastik!!!Naj:
Ngosha ze Swagga Don x4

Verse 1:(Fid Q)

Mc’z wanaenda down, ka Zim(babwe) dollars/
Mie sio bling, mie culture ka ZEMKALA/
Da brightest thang shining next to a diaMOND/
Ghost Writter ninapo Blaze ka AMO/
Mara nyingi mie nina bahati kama Lotto Machines/
Si mtu wa adventures kama Frodo kwenye Lord of the Rings/
Niite Roscoe, ninapoSPEAK in Tongues ka Jenkinz/
Don kama Bosco, Mad kama Ice Helsink/
Unataka Bed fight? Mie nina King size na French fries kwa Breakfast/
T- bone stake na PRISON BREAK kiGangstar/
Tattoo plan kama Michael Scolfield/
Bruce lee wa Rap ya Africa, Rock city naigeuza Rap City/
Nina Gucci Lips namaanisha ziko Brown/
Materialistic wanapenda niwe around/
Sexy & Single na pia hufurahi nikiwa FREE/
Nilipenda 3 sum zaidi ya unavyoipenda track hii/
Trust me, ninahitaji wife and some gorgeous Kids/
Seen, mie sio bogus we una dance ka Lotus juu ya hii beat/
Mashairi kwangu Pipi, nayagawa ka Santa Claus/
Kazi na Dawa Marco puff 3 kitu BOUNCE/
Mademu hawapendi kuona unavyomdiss FID/
nawaita Candy sababu they’re so SWEET/
I’m so 2010 sihitaji Pad or Pen,u so 2000 and late/
Na haulipuki ka Bin Laden/

Chorus:( Naj)
Ngosha ze Swagga don x82nd Verse:(Fid Q) My Mama.. didn’t raise no Fool/
Ninavyo Bust a Rhyme… wananiita Leader wa new School/
Ngosha ze SWAGGA DON..

Verse 2:

Uh uh usinidownload/
Hapa utapata ladha expensive zaidi ya iPhone/
Mie sio Superstar ni International I con/
I’m Internationaly known kama Tyson/
Flow iko so Universal kama yvone, CHAKA CHAKA/
Ladies and Gentlemen ni Rappers Rapper hapa/
Naweza kwenda Quick kama ROCKA nikawatisha kisha mkaa ‘’ We Love you FIDQ’’ U deserve girls… Q yuko stronger ka playa wa Baseball au Wrestling/
usiniite Paper Chaser mie nina Chase Dreams/
Kama una Pesa Jenga kabla haujaanza Pimp Rimz/
Jikomboe kama wanaojiunga na X treme/Drive with care, coz Life has no Spare/
na piiiiiiiiaaaaaaa…,.‘’

THEY SAY IM COOL LIKE FIRE & AND IM HOT LIKE ICE OH UYEAH… U FEEL WHAT I SPEAK COZ I SPEAK WHAT I FEEL OH YEAH’ X2

Saturday, June 12, 2010

JON B APANIA KUWAPANDISHA WASANII WA KASKAZINI

Produza Jon B anayepiga mzigo pande za R-chuga "Arusha" chini ya studio ya Grandmasters records amesema wasanii wa kanda ya kaskazini wana kila sababu ya kuhakikisha wanafanikiwa kutoka ingawa nguvu bado ni ndogo miongoni mwa wadau wa mziki huu wa kizazi kipya.

Akiongea na blog hii ya kitaa kwa ufahamu zaidi amesema kuwa wapo wasanii wenye uwezo na wanafanya vizuri lakini bado kanda ya kaskazini hatuna mtandao wa umoja kati ya wasanii, watangazaji, maproduza na wadau wa mziki.


Jon B

"Kitu muhimu ni kuwa na network itayotufanya tufahamiane vizuri na endapo kna jambo tunataka kulifanya basi tutashirikiana na kulifanikisha,ndio maana nimenzaa kukutfahumu wewe Wamilazo na wewe umenifahamu na nitaendelea kufahamiana na wengine. Alisema Jon B

Jon B ambaye pia aligusia wasanii wa kaskazini ambao wapo bongo, amesema haina haja leo hii ya kutoka huku kwetu na kwenda bongo wakati tuna uwezo ila tatizo ni sisi kutokuwa na mtandao wa kuhakikisha tunafahamiana na kusaidiana na kuwashawishi wengine haswa wasanii wenye majina kuja moshi kufanya kazi na kuchezwa.

Aidha, amesema kuwa kwa sasa tayari amefanya kazi kibao ambazo anatarajia kuziachia hivi karibuni na pia alikuwa katika mchakato wa kumalizia album ya John Walker na Ras Lion inayoitwa Sumu ya Panya kwa ajili ya kwenda sokoni.

Ni hayo tu toka R-chuga........................................................................................

UMESHAWAHI KUCHEZA MCHEZO HUU

Maisha siku zote huwa tofauti toka ulipokuwa mtoto hadi kfikia uzeeni. Hatua hii hupitia mambo mbalimbali haswa za kimechozo. Nakumbuka nikiwa mtoto tulicheza michezo mingi ya heshima tofauti na watoto wa sasa hivi ambapo usipokuwa makini wewe mzazi, mchezo wao ni ule wa baba na mama (kujenga magofa). Haya yote yanasemekana ni kutokana na utandawazi ambao huwajengea watoto ufahamu zaidi.


Huu ni mchezo wa Kuruka kamba ambao tuliucheza utotoni na pia kiafya una umuhimu. Michezo mingine ni Tikiri, Kombolele(Mchezo wa kujificha), Utengenezaji wa magari, Ndege wakati wa mavuno, Midoli ya kutengeneza, Kuendesha treli kwa kutumia betri ukiwa umechimba kijimtaro chiniKula mbakishie baba, Kuteneneza vitu mbalimbali kwa kutumia udongo, ukutiukuti,Kioo Kioo,Nage,Kujipikilisha....................................
Mingine nisaidie uzeee,nimesahau......!!!!!!!!

Tafakai juu ya mtoto wako ingawa sasa hivi tunaishi kizungu tunawanunulia vitu vya kuchezea ila wanavitumia ipasavyo au wanachunguzana miiili yao?....

UMEME KUKATIKA TANZANIA SIKU TATU

SHIRIKA la umeme nchini (Tanesco), limesema maeneo kadhaa katika mikoa 11 nchini yatakosa umeme kwa muda wa siku tatu kuanzia leo.

Mikoa hiyo ni Arusha, Tanga, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga, Mbeya, Morogoro, Tabora, Mara, Singida na Tanga.

Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud amesema hatua hiyo imechukuliwa kutokana na hitilafu iliyotokea katika mitambo ya Songas na kidatu, tatizo ambalo lipo nje ya uwezo wa shirika lake licha ya wataalamu kujitahidi kukabiliana na hali ili kuwapatia umeme wateja wake; hasa wakati huu wa michuano ya Kombe la Dunia inyaofanyika Afrika Kusini.

"Katizo hilo litakuwepo kuanzia Juni 12 -15, mwaka huu kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 5:00 usiku," alieleza Masoud katika hiyo.

Friday, June 11, 2010

MECHI ZA MWANZO FAINALI YA KOMBE LA DUNIA KUSHINDWA KUONESHANA UBABE

Mechi za ufunguzi wa fainali za kombe la dunia zilizoanza hapo jana, zimeshindwa kuoneshana ubabe baada ya kutoka sare.

Wenyeji wa mashindano ya Kombe la Dunia, Afrika Kusini, wameanza michuano hiyo kwa matumaini baada ya kutoka sare ya 1-1 na Mexico ingawa timu ya Mexico wenye uzoefu mkubwa wa kucheza katika Kombe la Dunia walianza kwa kumiliki mpira kwa kipindi kirefu, lakini walishindwa kumalizia nafasi zilizopatikana.

Baada ya mapumziko, kocha wa Afrika Kusini, Carlos Alberto Parreira, alifanya mabadiliko kwa kumtoa Lucas Thwala na kumwingiza Tsepo Masilela,mabadiliko yalizaa matunda wakati Siphiwe Tshabalala, kiungo wa Kaizer Chiefs, alipotikisa nyavu katika dakika ya 55 kuipatia Afrika Kusini goli la kuongoza.


Mchezaji wa Afrika kusini Siphiwe Tshabalala alipopiga shuti kali nakuipatia Afrika kusini goli la kwanza.

Goli hilo lilishangiliwa kwa mbwembwe zote zilizoambatana na dansi kavu kavu wakati wachezaji walipokusanyika pembeni.

Bahati mbaya kwa Afrika Kusini, kosa la kushindwa kuwakaba wachezaji wa Mexico katika eneo la hatari lilitoa fursa kwa Rafael Marques kusawazisha katika dakika ya 79.

Wakati hoho huo,Ufaransa na Uruguay zimetoka sare 0-0 kwenye mechi ya pili ya kundi A.

Uruguay walimaliza mchuano wakiwa wachezaji 10 baada ya Nicholas Lodeiro kupewa kadi nyekundu alipomchezea vibaya mlinzi wa Ufaransa, Bacary Sagna.

Ufaransa walifanya mashambulizi mengi bila mafanikio, na katika kipindi cha pili walifanya mabadiliko, akaingia nahodha wao Thierry Henry badala ya Nicholas Anelka, lakini lango la Uruguay likawa halifunguki.

Mkwaju mkali wa mshambuliaji wa Atletico Madrid, Diego Forlan, uliokolewa na kipa wa Ufaransa katika kipindi cha kwanza.


Hii ni moja kati ya mashambulizi kati ya timu ya ufaransa na Uruguay.

Michuano hiyo ya kombe la dunia inaingia katika siku ya pili ya kundi B, wakati leo Nigeria wanachuana na Argentina katika uwanja wa Ellis Park mjini Johanesburg ikifuatiwa na mechi kati ya Korea Kusini na Ugiriki.

Kocha wa Argentina, Diego Maradona, amesema anakusudia kuchezesha washambuliaji watatu dhidi ya Nigeria, na anatarajiwa kuwapanga mchezaji bora duniani, Lionel Messi wa Barcelona, Carlos Tevez wa Manchester City na mshambuliaji wa Real Madrid, Gonzalo Higuai.

Nigeria itawategemea washambuliaji wao wanaocheza Ulaya; nahodha Kanu Nwankwo anayeichezea Portsmouth, Yakubu Ayegbeni wa Everton, Obafemi Martins wa klabu ya Wolfsburg pamoja na Peter Osaze na Chinedu Obasi. Hii ni mara ya tatu kwa Kanu kushiriki Kombe la Dunia.

Tukutane baadaye katika ile pembe nne.......................................................




SAJNA NDANI YA JIJI LA WAJANJA

Msanii mchanga katika muziki wa kizazi kipya SAJNA kwa sasa yupo kwa wajanja jijini Dar toka Rock city "Mwanza" kwa lengo la kujitangaza zaidi na pia kuitangaza album yake ya kwanza ambayo iko katika hatua za mwisho kukamilika na itakuwa sokoni mwezi mmoja kuanzia sasa.


]
Album inaitwa IVETA, itakuwa na jumla ya nyimbo 10, baadhi ni IVETA, BINADAMU, MBALAMWEZI, SUBIRA, MGANGA, ROHO MBAYA, NADHIFA nk.Katika album hii atawashirikisha BELLE 9, LINAH na JOSEFLY.. Lengo la kuwashirikisha wasanii wachache ni kutaka kukionesha kipaji chake zaidi.

Studio zilizohusika kuipika album hii ni pamoja na TETEMESHA RECORDZ (Kid bwoy), AB RECORDS (Amba), MUSIC LAB (Duke), MZUKA RECORDS (Benja), A2P RECORDS (Sam Timba).

Kamua Dogo support utaipata kama utaonesha uwezo.

WANAFUNZI WA UDZUNGWA WAKIWA NDANI YA MOSHI FM

Wanfunzi wa chuo cha udzungwa Mountain Trust College wanaosoma mafunzo ya uanidhi na utangazaji, leo wametembelea kituo cha redio cha Moshi Fm kilichopo Moshi mjini kwa ajili ya mafunzo ya vitendo.

Chuo hicho ambacho kinatoa nafasi kwa wanafunzi kujifunza kwa vitendo kwa ajili ya kufahamu zaidi, lengo ni ili kuweza kakabiliana na changamoto za kazi watakapokwenda katika field.


Hawa ni wanafunzi wa udzugwa wakiwa ndani ya studio za moshi fm pamoja na mtangazaji Amina Mbwambo.

Chuo hiki kinatoa kozi mbalimbali kama Chuo hiki kinatoa kozi kama;-
Certificate and Diploma in Hotel Management-
Certificate in Early Childhood Department
-Communication Skills ( English, French, Spanish and Swahili for Foreigners)
-Certificate and Diploma in Tourism-Certificate and Diploma in Tour Guide and Driving
-Certificate and Diploma in Business Admistration
-Certificate and Diploma in Journalism.

Kwa kozi zote wanafunzi hujiunga na sehemu mbalimbali kwa ajili ya vitendo mfano hifadhi za taifa, hotel kubwa, Vituo vya Radio na Television,shule zenye viwango na pia hufanya safari za sehemu mbalimbali kwa ajili ya mafunzo zaidi.


Huyu ni Neema Mlay, mwanafunzi wa udzungwa anyesoma kozi ya uandishi na utangazaji ndani ya studio za moshi fm


Dickson mwanafunzi wa udzungwa nayesoma masomo ya utangazaji na uandishi ndani ya studio za moshi fm.


Irene mwanafunzi wa udzungwa anayesoma masomo ya utangazaji na uandishi ndani ya studio za moshi fm.


Sharifa Mndeme mwanafunzi wa udzungwa anayesoma masomo ya utangazaji na uandishi ndani ya studio za moshi fm.


Saumu Materu mwanafunzi wa udzungwa anayesoma masomo ya utangazaji na uandishi ndani ya studio za moshi fm.
Chuo kipo Moshi mjini mkabala na maktaba ya Kanisa la Katoliki la Kristo mfalme au kama uwezi kufika kwa mawasiliano zaidi ni +255 784 815 517 au +255 784 473 475 au kwa barua pepe ya udzungwamountaincollege@yahoo.com.
Fomu za kujiunga na masomo zinapatikana Moshi Fm Radio, Chuoni udzungwa na wewe uliye mbali piga simu ujulishwe kwa kupata fomu kwa shilingi 5000/=. Kwa wale wanaotoka mbali zipo hostel kwa ajili ya kulala. Jiunge wakati wowote kwani masomo yanaendelea.Kwa maelezo zaidi ya haya wasiliana au fika Udzugwa.
WAHI MAPEMA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


BAJETI 2010/11 YAANIKWA

SERIKALI jana imetangaza bajeti yake kwa mwaka wa fedha 2010/11 ambayo inaonekana kupunguza makali kwenye baadhi ya sekta huku ikiongeza makali kwenye maeneo mengine.

Bajeti hiyo ya Sh1.1 trilioni inaendelea kuweka kipaumbele katika uboreshaji miundombinu, elimu, afya, kilimo, na maji huku ikielekeza nguvu katika kubana matumizi ya serikali na ukusanyaji zaidi wa kodi,


Waziri wa fedha na uchumi Mstafa Mkulo

Kwa maelezo zaidi cheki magazeti ya leo.

TMK WANAUME YAVUNJIKA

Wasanii waliotengwa katika kundi la TMK wanaume halisi baada ya kuchaguliwa wasanii watano na Sir Nature watakaowakilisha kundi hilo wameamua kuanzisha kundi lao linalojulikana kwa jina la Wanaume.

Kampuni ya Mpo Afrika imetangaza kusaini mkataba na kundi jipya, likiundwa na wanamuziki kama Athuman Yahya (A.Man), Juma Mbelwa (Juma Jazz), Karim Kaiman (Kakaman), Abdul Ally (Mzimu), Richard Shauri (Rich One) pamoja na David Mpangile (Daz-p) walioachwa katika kundi la TMK Wanaume Halisi.


WAHUSIKA WALIOTENGENEZA KUNDI LA WANAUME

Hassan Umande amesema lengo la kuunda kundi hilo jipya ni kwa ajili ya kuendeleza sanaa na kuleta mabadiliko katika anga ya muziki wa kizazi kipya aka bongofleva hapa nchini.

Aidha ameongezea kuwa kuna vikwazo vingi vilivyotokea mpaka kuamua kujitenga ,yote hiyo kuepuka migongano ambayo kimsingi si ya lazima kwa sababu sote ni vijana na tunatafuta maisha,kwa hiyo kwa sababu tumetengwa basi tumeamua kuunda kundi la watu sita.

NI HAYO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Thursday, June 10, 2010

BONGO FLEVA NI SISTA DU?

Mwanamzuziki mkongwe katika game la mziki wa Bongo hip hop Jacob Makala a.k.a JCB amesema ngoma yake inayotamba hivi sasa ya “Bongo fleva” ina maana ya msichana ambaye hapendi kutulia na kushobokewa na kila mtu.

Akifafanua zaidi amesema kuwa mwanzoni kabisa wakianza game kulikuwa hamna bongo fleva ila walikuwa wanafanya hip hop (michano) ndio maana ukiuliza hip hop lazima utaje arusha.



Akihojiwa na Kituo kimoja cha Television nchini JCB amesema kuwa bongo hip hop ni mziki unaoeleza hali halisi ya kitaa yaani maisha kwa ujumla si bongo fleva mziki wa kusemana.

Akielezea malengo yake amesema kuwa sasa hivi ameamua kusimamam mwenyewe baada ya kutoa album tatu za kundi la Watengwa kama Iliandikwa, Fulu ile laana na Piga takatifu.

JCB amelonga kuwa yupo kwenye maandalizi ya kumalizia album yake ndani ya bongo (DSM) katika studio za Mj na Tongwa Records kwa ajili ya kufanyia mastering.

Aidha amesema album hiyo ina nyimbo 16 na bado yupo katika mchakato wa kutafuta jina baada ya kupata majina mawili “Makala ya makala na Kijiti” ili kuchagua ni jina ambalo litakuwa mzuka.

Ni hayo tu toka R-chuga.

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA

HISTORIA ya kombe iliandikwa kwa mara ya kwanza mwaka 1928 wakati Rais wa FIFA wakati huo, Jules Rimet alipoamua kuandaa michuano mikubwa zaidi duniani inayohusisha mataifa mbalimbali.

Ufunguzi wa michuano hiyo ilifanyika miaka miwili baadaye mnamo mwaka 1930 nchini Uruguay na timu 13 zilialikwa kushiriki michuano hiyo.Kuanzia hapo, FIFA ilifanikiwa kubadilisha miundo mbalimbali ya michuano katika miaka ya nyuma.

Timu 32 zinapatikana baada ya mchakato wa mechi za kufuzu ambazo zinashirikisha timu kutoka mataifa 200 duniani kote.Kabla ya kombe la dunia Mechi ya kwanza ya kimataifa ya soka duniani ilichezwa mwaka 1872 kati ya England dhidi ya Scotland ingawa katika kipindi hicho ilikuwa ni mara chache kwa mchezo wa soka kuchezwa nje ya Uingereza.

Hata hivyo, kuanzia mwaka 1900 mchezo wa soka ulipata umaarufu duniani kote na vyama vingi vya soka vikaanzishwa. Mechi ya kwanza rasmi ya kimataifa kuchezwa nje ya Uingereza ilikuwa kati ya Ufaransa na Ubelgiji ambayo ilichezwa Paris,Mei 1904.

Mchezo huo ulisababisha kuanzishwa kwa Shirikisho la soka duniani (FIFA) Mei 22, 1904. FIFA ilianzishwa na Vyama vya soka vya Ufaransa, Ubelgiji, Denmark,Uholanzi, Hispania, Sweden na Uswisi huku Ujerumani ikiomba kujiunga.


Huku mchezo wa soka ukianza kupata umaarufu, mchezo huu ulianza kutambulika kama mchezo rasmi wa michezo ya Olimpiki mwaka 1904 katika kipindi cha majira ya joto.Baadaye FIFA ilikuja kusimamiamichuano ya Olimpiki katika upande wa soka mnamo kipindi cha majira ya joto mwaka 1908.

Wakati huo mchezo wa soka ulikuwa unajumuisha wachezaji wa ridhaa tupu na ulikuwa unachukuliwa kama mchezo wa maonesho tu kuliko ushindani.

Timu ya taifa ya soka ya ridhaa ya England ilishinda michuano hiyo ya Olimpiki mwaka 1908 pamoja na ile ya mwaka 1912.Baadaye FIFA ilijaribu kuanzisha michuano mingine ya soka ya kimataifa bila ya kuhusisha michuano ya Olimpiki.

Majaribio haya yalianzishwa mwaka 1906 nchini Uswisi.Hizi zilikuwa siku za mwanzo za soka la kimataifa na historia rasmi ya FIFA inaelezea kwamba mkutano huo ulishindwa kuzaa matunda.

Huku michuano ya Olimpiki ikiendelea kushindanisha timu za ridhaa, michuano ya timu za kulipwa nayo ikaanza.Michuano ya Torneo Internazionale Stampa Sportiva, ilifanyika jijini Turin, Italia mwaka 1908. Hii ilikuwa ya kwanza kabisa na mwaka uliofuata Sir Thomas Lipton alianzisha michuano iliyofahamika kama ‘Kombe la Sir Thomas Lipton’ iliyofanyika Turin.

Michuano hiyo ilikuwa inashirikisha klabu na si timu za taifa. Klabu moja ilikuwa inawakilisha taifa zima nyumbani. Kwa sababu hii, hakuna michuano ambayo ilichukuliwa kama mfano wa kombe la dunia kabla yauwepo wa kombe la dunia.

Mwaka 1914, FIFA ilikubali kuitambua michuano ya Olimpiki kama ‘Michuano ya dunia ya ridhaa’ na ilikubali kuwajibika kuandaa michuano hiyo.Hii ilisababisha iwepo michuano ya kwanza ya kimataifa ya soka katika Olimpiki ya mwaka 1920 ambapo Ubelgiji alichukua.Uruguay ikashinda michuano yaOlimpiki ya mwaka 1924 na 1928.

Mnamo mwaka 1928 FIFA ilichukua uamuzi wa kuandaa michuano yao wenyewe.Huku Uruguay ikiwa imeshinda mara mbili michuano ya Olimpiki na ikijiandaa kusheherekea mwaka mmoja baada ya kupata uhuru, FIFA iliamua kuipa Uruguay uenyeji wa michuano hiyo ya kwanza ya kombe la dunia 1930.Michuano ya kwanza ya kombe la dunia

Michuano ya mwaka 1932 ya kipindi cha majira ya joto ilifanyika jijini Los Angeles na haikupanga kuujumuisha mchezo wa soka kutokana na umaarufu mdogo wa mchezo wa soka Marekani.

FIFA na IOC zilikuwa zimeshindwa kukubaliana masuala fulani ya michuano hiyo, kwa hiyo mchezo wa soka ukaondolewa katika orodha ya michezo ya mwaka huo.

Rais wa FIFA, Jules Rimet ndiye akaamua kuandaa michuano hiyo iliyofanyika Uruguay mwaka 1930.Vyama kadhaa vya soka viliteuliwa kupeleka timu zao na huku chaguo la uenyeji likienda kwa Uruguay. Hiyo ilimaanisha kuwa timu nyingi za Ulaya zingelazimika kukatiza Bahari ya Atlantic kucheza michuano hiyo.

Hakuna timu yoyote ya Ulaya ambayo ilithibitisha kupeleka timu mpaka ilipobaki miezi miwili kabla ya kuanza kwa michuano hiyo.Kwa juhudi binafsi za Rimet alifanikiwa kuzishawishi nchi za Ubelgiji, Ufaransa, Romania na Yugoslavia kusafiri.

Kwa ujumla nchi 13 zilishiriki michuano hiyo huku saba zikitoka Amerika Kusini,nne kutoka Ulaya na mbili kutoka Amerika Kaskazini.

Mechi mbili za kwanza zilichezwa mfululizo huku Ufaransa ikiichapa Mexico 4-1 na Marekani ikiichapa Ubelgiji 3-0.Bao la kwanza katika historia ya kombe la dunia lilifungwa na Lucien Laurent wa Ufaransa.

Siku nne baadaye dunia ilishuhudia Bert Patenaude akifunga mabao matatu kwa mpigo (Hat trick) katika ushindi wa 3-0 wa Marekani dhidi ya Paraguay.Katika pambano la fainali lililochezwa Montevideo, wenyeji Uruguay waliichapa Argentina 4-2 mbele ya mashabiki 93,000 na kuingia katika historia ya timu iliyotwaa kwa mara ya kwanza taji holo.


Hivyo ndivyo michuano ya kombe la dunia ilivyoanza.





Madiba akifurahia kombe la dunia. Hongera!!!!!

Je wajua haya kuhusu kombe la Dunia?


-Michuano ya kombe la dunia imechezwa mara 17 lakini mpaka sasa ni nchi sita tu zilizowahi kutwaa kombe hilo.

-Mechi ambayo ilihudhuriwa na mashabiki kidogo zaidi katika kombe la dunia ni kati ya Romania na Peru katika fainali za mwaka 1930 nchini Uruguay. Waliingia mashabiki 300 tu.

-Hakuna nchi yoyote ya Ulaya iliyowahi kutwaa kombe la dunia nje ya bara la Ulaya.

-Diego Maradona ndiye mchezaji aliyecheza mechi nyingi akiwa na kitambaa cha unahodha. Alicheza mechi 16 kama nahodha.

-Fainali za kombe la dunia mwaka 2002 ziliandaliwa katika nchi za Japan na Korea Kusini. Ugomvi mkubwa baina yao ulikuwa ni jina la nchi gani litokee kwanza katika tiketi za mechi hizo.

-Hakuna nchi yoyote ambayo iliwahi kufungwa pambano lake la kwanza na kutwaa kombe la dunia.

-Julai 31 imetajwa kama siku ya mapumziko nchini Uruguay baada ya taifa hilo kutwaa kombe la dunia lilipofanyika mara ya kwanza.

-Tabia ya wachezaji kubadilishana jezi uwanjani ilipigwa marufuku mwaka 1986 na FIFA kwa sababu haikupenda kuwaona wachezaji wakitoka nje ya uwanja vifua wazi.

-Matokeo mengi katika kombe la dunia ni yale ya 1-0
Rigobert Song wa Cameroon ndiye mchezaji aliyepewa kadi nyekundu katika michuano miwili ya kombe la dunia mfulilizo. Alipewa dhidi ya Brazil mwaka 1994 na akapewa dhidi yaChile mwaka 1998.

-Mchezaji aliyefunga mabao mengi ya kichwa katika fainali za kombe la dunia ni Miloslav Klose wa Ujerumani.Katika fainali za mwaka 2002 alifunga mabao matano kwa kichwa.

-Pambano la kombe la dunia mwaka 1970 kati El Savador na Honduras lilikuwa na upinzani mkubwa kiasi kwamba nchi hizo ziliingia katika vita ya mtutu kwa siku tatu.

-Ni mabara mawili tu ambayo yamewahi kushinda kombe la dunia,hayo ni Ulaya na Amerika Kusini.Ulaya imeshinda mara nane na Amerika Kusini imeshinda tisa.Mabara ya Asia, Afrika, Amerika Kaskazini na Kati yote yameshindwa kutwaa taji hili.

-Brazil ni nchi pekee iliyocheza michuano yote ya fainali za kombe dunia.

-Brazil ndiyo nchi pekee iliyofunga idadi kubwa ya mabao katika fainali za kombe la dunia. Imefunga mabao 173.

NCHI ZILIZOTWAA KOMBE LA DUNIA 1930 HADI 2006


1930 Ilifanyika Uruguay, fainali ni kati ya Uruguay vs Argentina 4-2

1934 Ilifanyika Italia, fainali ni kati ya Italia vs Czechoslovakia 2-1

1938 Ilifanyika Ufaransa, fainali ni kati ya Italia vs Hungary 4-2

1950 Ilifanyika Brazil, fainali ni kati ya Uruguay vs Brazil 2-1

1954 Ilifayika Uswisi, fainali ni kati ya Ujerumani vs Hungary 3-2

1958 Ilifanyika Sweden, fainali ni kati ya Brazil vs Sweden 5-2

1962 Ilifanyika Chile, fainali ni kati ya Brazil vs Czechoslovakia 3-1

1966 Ilifanyika England, fainali ni kati ya England vs Ujerumani 4-2 (pen)

1970 Ilifanyika Mexico, fainali ni kati ya Brazil vs Italia 4-1

1974 Ilifanyika Ujerumani, fainali ni kati ya Uholanzi vs Ujerumani 1-2

1978 Ilifanyika Argentina, fainali ni kati ya Argentina vs Uholanzi 3-1 (pen)

1982 Ilifanyika Hispania, fainali ni kati ya Italia vs Ujerumani 3-1

1986 Ilifanyika Mexico, fainalili ni kati ya Argentina vs Ujerumani 3-2

1990 Ilifanyika Italia, fainali ni kati ya Ujerumani vs Argentina 1-0

1994 Ilifanyika Marekani, fainali ni kati ya Brazil vs Italia 3-2 (pen)

1998 Ilifanyika Ufaransa, fainali ni kati ya Brazil vs Ufaransa 0-3

2002 Ilifanyika Korea/Japan, fainali ni kati ya Ujerumani vs Brazil 0-2

2006 Ilifanyika ujerumani, fainali ni kati ya Italia vs Ufaransa 5-3 (pen)

Fainali hizi ni mara ya kwanza kuchezwa katika bara la afrika ingawa zipo baadhi ya timu za taifa kutoka afrika zikishiriki. Michuano hii itafunguliwa na raisi wa kwanza wa Afrika kusini na kushuhudiwa na viongozi wakubwa duniani kama Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Kin Moon. Makundi ambayo yanategemewa kukipiga tarehe kumi na moja mwezi huu kule Afrika kusini ni kama ifuatavyo;


Kundi A. Afrika Kusini, Mexico, Uruguay na Ufaransa.
Kundi B. Argentina, Nigeria, Korea Kusini na Ugiriki.
Kundi C. England, Marekani, Algeria na Slovenia.
Kundi D. Ujerumani, Australia, Serbia na Ghana.
Kundi E. Uholanzi, Denmark, Japan na Cameroon.
Kundi F. Italia, Paraguay, New Zealand na Slovakia.
Kundi G. Brazil, Korea Kaskazini, Ivory Coast na Ureno.
Kundi H. Hispania, Uswisi, Honduras na Chile.


Viwanja vya Afrika kusini vitakavyokuwa na shughuli.

Cheki vikosi vitakavyoumana kuanzia tarehe 11.06.2010










Ni hayo tu kwa leo kwa lengo la kukumbusha wapi tumetokea na wapi tunaelekea na nini vinatokea katika mchakato wote wa kombe la dunia.
Tucheki kwa raha zetu....................................................................................................!!!!!!



Monday, June 7, 2010

TAIFA STARS 1 - BRAZIL 5

Timu ya taifa ya Tanzania, Taif Stars, imepaia kichapo cha magoli 5-1 katika mechi ya kujipima nguvu iliyofanyika Jana jioni katika uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.

Mshambuliaji Robinho ndiyo aliwapatia Brazil goli la kwanza, kabla ya kuongeza la pili kwenye mechi ambayo si makosa kusema Taifa Stars walicheza vizuri ingawa tatizo la kawaida limekuwa likijirudia - kukosekana kwa maarifa ya kufunga.


Kaka akitoa dole tu......!!!!

Shambulio la Kaka na mengine mawili kutoka kwa mchezaji wa akiba, Ramires yalikamilisha magoli kwa The Selecao, lakini Stars walionekana kuwachokoza Brazil ambapo katika dakika ya sita Mrisho Ngassa alikosa goli la wazi.

Taifa Stars walipata goli la kufutia machozi kupitia Jabir Aziz, mchezaji wa akiba aliyemalizia kwa kichwa mpira wa kona.

Mchezaji muhimu aliyekosekana ni mlinda mlango namba moja Julio Cesar aliyejeruhiwa katika mechi ya majaribio dhidi ya Zimbabwe juma lililotangulia, badala yake alicheza mlangoni alicheza Heurelho Gomes.

Tukaze buti tutaweza................................................