Saturday, June 19, 2010

DHAHABU YA KASKAZINI

Kila kukicha tunategemea kuona mziki wa Tanzania unawanufaisha wasanii wa kitanzania na kufika nlevel za kimataifa kwa lengo la kujulikana huku wasanii wanachipikua tukitegemea pia kufanya vizuri.

Kanda ya kaskazini ni moja kati ya kanda zenye wasanii wazuri Tanzania, lakini kilio chao ni kukosa air tym haswa kwa redio za Dar na kutoaminiwa kwa studio za mikoani kuwa zinafanya vizuri huku wasanii hawa wakipata changamoto ya kukosa ushirikiano baina yao.



Suleiman Zitueni “Top B” a.k.a Dhahabu ya kaskazini ni mmoja kati ya wasanii wanaofanya vizuri kanda ya kaskazini ila si msanii mchanga wa la wa juu bali wa kati anyefahamika katika mziki wa kizazi kipya.

Kila mtu anayo hatua ya maisha kama alivyo msanii huyu akielezea hatua ya aliyopiga mpaka alipofikia katika mziki huu wa kizazi kipya.

Top B anasema alianza mziki mwaka 2005 ndani ya mkoa wa Kilimanjaro,moshi mjini kama msanii wa kujitegemea na jina hili alipewa na mama yake.

“Top B lina maaana ya Top in bongo fleva na jina hili nilipewa na mama yangu baada ya kutiririka ma freestyle kila kukicha ndio akaniambia hakika mwanangu utakuwa top katika mziki huu” alisema Top B

Anasema rekodi ya kwanza katika game ilikuwa inaitwa Kifaa, kazi ilishonwa 360 production kwa produza Wise Mad studio toka pande za huku ingawa ngoma hii haikupata air time ya kutosha.

Ngoma hii ndio ilianza kumtambulisha na kuanza kujulikana katika ukanda wa kaskazini ingawa redio zilikuwa mbili Kibo Fm na Kili Fm ila ngoma ikaendele kugongwa kiaina.

Baada ya safari hii ya kutambulika, Top B anasema alipata nafasi ya kujiunga na kundi la mzizini camp, kundi lilokuwa na nguvu kipidi hicho baada Meneja wa kundi hilo Bw. Kalage kumuita.
“Meneja baada ya kunisikia aliniomba nijiunge na kundi hilo na alinichagua kuwa kiongozi na washkaji tuliokuwa nao ni Rhymes B,Ommy, Bilo one na Kupa.” Alisema Top B



Baada ya wiki moja tuliondoka kwenda Dsm kufanya album ya kundi katika studio za Metro studio chini ya mkono wa Allan Mapigo na Big tyme kwa Comoriel na kufanya rekodi sita kama watanzania ya Rhymes, Rudi mpenzi ya kupa,wachakusita ya Bilo one na nyingine.

“Ukweli mimi sikufanya ngoma hata moja zaidi ya kujazia sauti yaaani vile viitikio (back vocal) ila ngoma moja ya Rhymes B inaitwa sikiliza nilipata nafasi kidogo kuweka viji mistari kidogo maana nilifika wiki moja tukaenda dsm wakiwa tayari wameshajiandaa” alisema Top B.

Baada ya kurudi Mji wa wagumu “Moshi” tukasikiliza ngoma tulizofanya, wakasikiliza ngoma inaitwa “sikiliza” ambayo nilipata shavu nene kidogo na niligonga na Rhmes B, nikawa nimefanya poa,ikabidi turudi Dsm kwa Comoriel na kuirudi na nikapata verse.

Ujio kutoka bongo kwa mara nyingine, walisikia studio ya MO-TOWN RECORDS na kupanga kuitembelea ili kujua kazi zinavyokwenda ila siku hiyo Top B anasema hakwenda kwa ajili ya majukumu ya home.

Ndani ya MO-TOWN RECORD walikutana na produza Tripple A na kuwapa ofa ya ngoma moja bure na kuanza kazi ya kugonga beat tyme hiyo.

“Machizi baada ya kupata ofa walinicallm, nikatimba na nilikuwa na ngoma yangu iliyoitwa usiondoke, tukagonga beat then tukarudi skani kwa ajili ya kupangana katika verse” Alinitonya Dhahabu ya kaskazini.

Walijipanga kama kundi la watu wanne na kushambulia ngoma hiyo ya kwanza katika kundi ingawa wapo watu hawakusikika katika ngoma hii ya usiondoke.

“ Sijui sababu ni nini…..Meneja aliwatoa Kupa na Ommy katika ngoma hii na Bilo One aliyekuwa Dsm alikuja na kufanya vocal, so tulirudia tena ile ngoma kwa mara ya pili” Alisema Top B.

“ Produza alituahidi baada ya muda mchache tutaipa, nakweli ikawa hivyo na kuipeleka redio na ni kati ya ngoma kali zilizotesa kanda ya kaskazini na kundi la mzizini kujulikana baada ya kuachiwa nikiwa nashika verse ya kwanza na chorus” alinena Top B
.


Mchizi alijulikana na kupata makubaliano ya kuwa chini ya studio ya MO-TOWN RECORDS kwa ajili ya kufanya album.

“Nilitamani sana kufanya kazi zangu mwenyewe, so nilifurahi na kukubali makubaliano hayo na nikarudia ile nyimbo ya kifaa” Alisema Top B.

Akazidi kumwaga mavocal katika studio hiyo na kugonga UNAJUA akimshirikisha Voice wonder, ZEINA alisimama mwenyewe, RIZIKI POPOTE akimpa shavu Ras Lion na NAKUTHAMINI akigonga na Muddy best.

Baadhi ya ngoma zilipata air time yakutosha na kumtambulisha na kuwa msanii wa kati ambaye anafahamika na baadhi ya watu Tanzania huku ukanda wa kaskazini akiuteka zaidi.

“Nilipata support kwenye baadhi ya redio ila ngoma ya mwisho ya NAKUTAHAMINI haijapata air tym kwa redio za nje ya kanda ya kaskazini na nilipata nafasi ya kufanya video ya UNAJUA pale Empty soulz kwa Osama, video ambayo ndio ilifanya nijulikane na watu wanaonikubali” alisema Top B.

Kwa sasa Msanii huyu amekuwa kimya baada ya kuachia ngoma yake mwezi wa kwanza mwishoni ila maandalizi ya album yapo jikoni huku akitafakari jina la album hiyo.

“ Nategemea kumaliza album yangu, niitangaze ili kwenda sokoni kama ahadi yangu kwa mashabiki wangu na sitaishia hapa ila niwe msanii wa kimataifa na mwenye kujali sanaa ya mziki”

“ Watanzania nawashauri watoe sapoti kwa wasanii na mziki wa bongo fleva na pia wasanii wawe makini kwenye kazi yao isipuuzwe, Nawapenda wote, saaaana saaaana” Alimalizia kwa kusema hayo Top B.

Hii ni hatua ya msanii huyu wa mziki wa kizazi kipya katika mziki wa kizazi kipya na nitakuwa nakufahamisha wasanii wanaofanya vizuri haswa wale wachanga.

Ni hayo tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


No comments:

Post a Comment