Monday, June 7, 2010

KIKWETE NDANI YA MOSHI LEO KWA ZIARA YA SIKU 3

Rais Jakaya kikwete leo anafanya ziara kwa mara nyingine tena mkoani kilimanjaro, ambapo atazindua tawi jipya la benki ya biashara la Kenya –KBC,lililopo mjini moshi.


Hamjambo wananchi wa kilimanjarooooooo!!!!

Kwa mujibu wa taarifa ya mkoa wa Kilimanjaro, kesho atafungua mkutano wa mameya wa jiji, miji, wenyeviti na wakurugenzi wa halmashauri za wilaya, utakaofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha polisi mjini moshi.


Rais Kikwete (Katikati) ndani ya vazi la chama tawala na ishara ya chama(kidole gumba).

Katika ziara hii, Raisi anatarajiwa kufungua ofisi mpya za makao makuu ya jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro na baadae kuutembelea mradi wa kusambaza maji wa himo, sanjari na kugawa kadi kwa wanachama wapya wa CCM.

No comments:

Post a Comment