Saturday, June 5, 2010

BWANA CHUCHU AFARIKI DUNIA


Bwana chuchu na kingwendu


Bwana chuchu kushoto.

Aliyekuwa mmiliki wa Band ya chuchu sound,Mkurugenzi wa chuchu radio Yusuph Chuchu na Heratbeat records vilivyopo Zanzibar, amefariki dunia jana jijini Nairobi, mazishi yanafanyika leo visiwani Zanzibar. R.I.P Babu chuchu!!

Yussuf Ahmed Alley alijipatia umaarufu mkubwa miaka ya mwanzoni mwa 2000 na bendi yake ya Chuchu Sound,iliyokua na wakali kama Mao Santiago,Omary Mkali,Waziri Sonyo,marehemu Gabby Katanga na wengine kibao,hasa na kibwagizo cha ''EEH..KWAHERI'' kwenye miondoko ya mduara.

Haijajulikana mara moja chanzo cha kifo chake.Msiba upo Kisima Majongoo na Mazishi yanafanyika kwenye makaburi ya MwanaKwerekwe leo saa 10,kisiwani Zanzibar.

Ina lil laahi wa inna ilayhi rajjoun.......................!!!!

No comments:

Post a Comment