Friday, June 4, 2010

JIULIZE

Kwa nini upendo hushamiri wakati wa urafiki kuliko mnapoamua kuishi wawili!!!!!!!!!!!!!!!!




CHOCOLATE



PERFUME




FLOWER

Mara nyingi katika maisha ya sasa hivi ( dot com) huwa vijana hutafuta wenyewe wachumba. Ila wakati unavyozidi kwenda hata vijana wenye umri wa kati hutafuta marafiki yaaani wapenzi na moja kwa moja hujiingiza katika ngono zembe.


Kipindi hiki huwa mapenzi yanakuwa yako juu kama obama au yanashamiri na kujenga mizizi kama ya mbuyu. Hapo ndipo manjina mazuri saaaaaana wanakuwa wanaitana sweet,dear,my lotion,darling,my luv,precious,baby,honey,my carpert,my side,my sweet potatoes,my sugar banana,. Mbali na hapa huwa wanananunuliana zawadi kila mar,zawadi za nguo za aina mbalimbali,maua,kadi,chocolate,perfume,ice cream,pipi,biscuts na vingine vingi haswa vile vya kitoto najua unavifahamu bila kusahau simu kwa sana na ujumbe mfupi wenye maneno matamu ya mapenzi.

Malengo yakishatimia ya kuishi pamoja iwe kwa ndoa au tumeamua vitu hivi huyeyuka kama barafu kwenye jua. zawadi hamna,jina utaitwa lako la kuzaliwa au kama mna mtoto atakuita mama au baba mwang'onda.

Nimejiuliza kuwa baada ya kufanikiwa kuingia ndani nakuwa mwili mmoja naamini furaha lazima izidi saana na upendo uongezeke. ILa cha kushangaza upendo wa kawaida tofauti na urafiki.

Jaribu kujiuliza kisha jaribu kuimarisha upendo na mume au mke wako kama awali.

Ni hayo tu wandugu. Habari ndo hiyo!!!!!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment