Tuesday, June 22, 2010

AFRIKA BYE BYEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Wenyeji wa kombe la dunia, Afrika Kusini wametupwa nje ya fainali za kombe la dunia pamoja na kwamba walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ufaransa katika mechi yao ya mwisho.
Hata hivyo Vigogo wa ulaya Ufaransa wameliaga kombe la dunia wakishika mkia kwenye kundi baada ya Afrika Kusini kuwabebesha virago.
Wawakilishi wengine wa Afrika, Nigeria watabidi wajilaumu wenyewe kwa kuliaga mapema kombe la dunia, kutokana na nafasi nyingi za wazi walizozipoteza.
Nigeria ilihitaji ushindi kwenye mechi yake dhidi ya Korea Kusini, lakini iliambulia sare ya magoli 2-2, yalifungwa na Kalu Uche kwenye dakika ya 12 na Yakubu kwa njia ya penalti kwenye dakika ya 69.
Matumaini ya Afrika yamebaki kwa timu za Algeria, Ghana na Ivory Coast.

No comments:

Post a Comment