Monday, June 7, 2010

MAENEO YA WAZI YAWA DAMPO KATA YA PASUA

Maeneo ya wazi katika kata ya pasua yamekuwa dampo baada ya kukosa sehemu maalumu ya kuweka taka wakati mpango wa ukusanyaji taka ukipingwa na wananchi.

Katika maeneo ambayo manispaa iliweka mankotena imekuwa ikilalamikiwa na wananchi haswa kutokuwepo kwa mankotena hayo na mengine kutoondolewa pindi yanapojaa takataka.

Moja kati ya eneo katika kata ya pasua ni eneo la wazi katika mtaa wa majengo mapya ambalo kwa sasa limekuwa eneo la kutupa taka na kuwa hatari ya milipuko ya magojwa. Eneo hili limenzungukwa na nyumba kitu ambacho ni hatari haswa kwa watoto wanaopenda kucheza eneo hilo




Hili ndio eneo la wazi la mtaa wa majengo mapya ambalo limekuwa sehemu ya kutupia taka (jalala).

Hii ni changamoto kwa viongozi husika kupambana na hali hii kuepuka na magojwa ya milipuko na maeneo haya ya wazi kubaki na kazi ambayo ndio lengo lake.

Think about it!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!





No comments:

Post a Comment