Monday, June 7, 2010

UFAGIO KWA WAFANYABIASHARA MOSHI

Mkutano wawaponza wafanyabiashara.

Mameya, wenyeviti na wakurugenzi wa halmashauri za wilaya nchini,wanatarajiwa kukutana katika mkutano mkuu wa jumuiya ya Tawala zamikoa na serikali za mitaa-ALAT, unaokutana mjini Moshi Juni 9 hadi 10 mwaka huu.

Hali ya sasa moshi haswa katika maeneo yaliyozeeleka kwa wafanya biashara yamekuwa meupe. mfano mbele ya kituo cha polisi,kona ya mawenzi hospitali na karibu ya NMB bank ndio maeneo maarufu kwa wafanyabiashara wa viatu,soksi,mapazi,shuka na taulo.



Hali ndivyo inaonekana kwa sasa katika manispaa ya moshi.

Baadhi ya watu wamesema kuwa maeneo hayo huwa hayaruhusiwi kufanya biashara lakini kwa kipidi cha nyuma watu wamekuwa wakifanya biashara katika maeneo hayo. Hivyo basi, mkutano huu na Maneno ya Mkurugenzi wa halmashauri ya moshi ya kuweka mji safi inasemekana ni sababu ya mkutano huu.


Hili ni gari la halmashuri likiwa limemkamata Mfanyabiashara.

Hali ya jana kwa wanagambo walikuwa watendaji kwa kuwakamata na kuwakimbiza wafanyabiashara na bidhaaa zao. Hali hii imekuwa gumzo katika manispaa hii kwa wafanyabiashara kukaidi kwenda memorial(eneo ambalo limetengwa) kwa madai eneo hilo halina maandalizi na biashara bado ni changa.



Hawa ni wanamgambo wakimkimbiza mfanyabiashara wa viatu.

Ni changamoto kwa wahusika kulifanyia kazi ili kuachana na malumbano na wafanyabiashara haswa kwa kukaa pamoja na kufika muufaka. Maana hapa yapo mengi ya kujiuliza.

Ni hayo tu waungwana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.

No comments:

Post a Comment