Friday, June 4, 2010

PESA NA MAPENZI KIPI MUHIMU KWA SASA.


Kwa maisha ya sasa pesa na mapenzi kipi hutangulia.


v/s



Kipindi cha nyuma wazazi wetu walitafutiwa wachumba na bibi na babu zetu haswa kwa kuangalia vigezo vingi ila kikuu ni tabia,ukoo na kabila.
Muda ulivyozidi kwenda dunia ya jana na ya leo ni tofauti sana, sijui na kwa ajili ya utandawazi au ni nini………..?.

Watu wapo katika mfumo tofauti wa kutafuta yule anayempenda mwenyewe ingawa kunakuwa na uchaguzi mbaya kwa baadhi ya watu kutokana na tamaa ya kumuona mtu kwa mwonekano wa nje kwa kudhani anzo hela au kwa kuangalia fedha.

“HAPENDWI MTU LINAPENDWA POCHI” ni usmeni wa vijana wengi sana wakike au wakiume. Wanawake leo hii hawezi kuwa na mtu asiye na hele tena kwa kunjua anafanya kazi gani na wazazi nao huuliza mchumba wako anafanya kazi gani yupo vipi kifedha na wanaume huwakimbilia mashuga mumy wenye fedha kwa ajili ya kulelewa.

Ndoa nyingi za sasa inasemekana hazidumu na zikiorodheshwa sababu nyingi kama kusalitiana (kuna mambo mengi humu…!!!),hali ngumu ya maisha,kukurupuka kuoa mtu asiyechaguo lako na mengine. Ila hali ngumu ya maisha imekuwa kigezo cha watu kutafuta wenza wenye uwezo ili maisha yao yaende vizuri.

Jaribu kujiuliza, siku ya kwanza unapomfata msichana au shuga mumy anapokupenda atakuonyesha manjonjo yote kuhusu hela ndipo hapo watu hulegea na kujua bukheri imefika. Yote ni kutokuwa na ajira.

Jaribu kujiuliza tena,Mapenzi ya sasa bila fedha kuna kupendwa kweli!!!!!!

Ni hayo tu wandugu,majibu nitayapata kwenu.

No comments:

Post a Comment