Thursday, June 3, 2010

UTAPANDA AU KUENDESHA PIKIPIKI!!!!!!!!!!!!!!!

Ajali inaua,inajeruhi:usishabikie mwendo kasi:mpanda pikipiki vaa kofia ngumu!

Watu 181 wamefariki dunia kwa ajali za pikipiki katika ajali 1,414 zilizotokea kote nchini katika kipindi cha miezi minne kuanzia Januari, huku zikiacha majeruhi 1,206, imeelezwa.

Akizungumza juu ya mabadiliko ya tarehe za kuadhimisha Wiki ya Usalama Barabarani, Mwenyekiti wa baraza linalosimamia masuala hayo, Abbas Kandoro alisema ajali nyingi zinatokana na abiria kushabikia mwendo wa kasi na wengi kutovaa kofia za kujikinga kichwa.

Kandoro, ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Mwanza,alisema ndio maana kaulimbiu ya mwaka huu ni "ajali inaua, inajeruhi; usishabikie mwendo wa kasi; mpanda pikipiki vaa kofia ngumu" ambayo alisema inalenga kuwaelimisha wapandaji wa usafiri huo kuwa makini.

Aliongeza kwa kusema ongezeko hilo la ajali linaonekana kwenda sambamba na ongezeko la vyombo hivyo vya usafiri, ambavyo katika mwaka mmoja uliopita pikipiki zimekuwa moja ya vyombo vinavyotegemewa sana kwa usafiri wa abiria.

TUWE WAANGALIFU NA VYOMBO VYA MOTO HAVINA URAFIKI

No comments:

Post a Comment