Saturday, June 5, 2010

MATUMANI YA DROGBA KUONEKANA



Nahodha wa Ivory Coast, mshambuliaji hatari wa Chelsea ya Uingereza, Didier Drogba, amelazimika kufanyiwa operesheni ya dharura kwenye mkono wake wa kulia baada ya kuvunjika mfupa kwenye kiwiko chake.

Drogba alivunjika mkono katika mechi ya kirafiki dhidi ya Japan ambapo Ivory Coast ilishinda kwa mabao 2-0.Drogba aliifungia timu yake bao la kuongoza kabla ya kuchezewa rafu mbaya na beki wa Japan, Tulio kwenye dakika ya 19 ya mchezo huo uliochezwa nchini Uswizi.

Kuumia kwa Drogba ni pigo kwa Ivory Coast ambayo imepangwa kundi la kifo pamoja na Brazili na Ureno.

Akiongea wakati akiwahishwa hospitali kwa matibabu zaidi, Drogba amesema kwamba ndoto yake ya kung'ara kwenye kombe la dunia imeyeyuka kwani hataweza tena kuiwakilisha nchi yake kama alivyopanga.

Lakini baada ya ushauri wa madaktari na operesheni atakayofanyiwa usiku huu, Drogba amesema kwamba amepata matumaini ya kurudi uwanjani kuiwakilisha nchi yake kwenye kombe la dunia ila hajui kama atamudu kulisakata kabumbu vizuri.

Akiongelea hali ya Drogba, kocha wa Ivory Coast Sven-Goran Eriksson amesema kuwa hali halisi ya Drogba itajulikana kesho baada ya ripoti ya madaktari

No comments:

Post a Comment