Sunday, June 6, 2010

DOGO MASANJA a.k.a MAZIMU

Katika safari ya maisha daima huwa na historia pana kwa kufahamu na kukutana na mambo mengi. Mchizi anajulikana kwa jina la YUSUPH MICHAEL MAZIMU (Masanja Jr) ni mtangazaji wa redio Moshi Fm na anasukuma book pande za MUCCOBS. Ukipenda kumsikiliza bafya 90.2 Moshi Fm mida ya saa 5 asubuhi katika show ya Movement Amplified.


Masanja Jr; Anabofyaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!

Dogo anablog inayojulikana kwa jina la www.mazimu11.blogspot.com kama vipi kacheki ishuz pande hizo.

TAFAKARI KWA HILI

Tunakila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kutujalia pumzi na uzima ndio maana leo tumeweza kukutana tena na kupeana michapo ya leo siku ya jumapili. Kidogo tu nilichowaandalia waungwana ni kuwa kila sekunde ya maisha inavyosogea tunapaswa kutafakari mambo mengi sana.

Ila leo naomba tutafakari juu ya hii picha kisha tukipata majibu tunaweza kujuza.


Jumapili njema yenye mafanikio nafuraha na tukumbuke kutoka na familia zetu.

Saturday, June 5, 2010

MATUMANI YA DROGBA KUONEKANA



Nahodha wa Ivory Coast, mshambuliaji hatari wa Chelsea ya Uingereza, Didier Drogba, amelazimika kufanyiwa operesheni ya dharura kwenye mkono wake wa kulia baada ya kuvunjika mfupa kwenye kiwiko chake.

Drogba alivunjika mkono katika mechi ya kirafiki dhidi ya Japan ambapo Ivory Coast ilishinda kwa mabao 2-0.Drogba aliifungia timu yake bao la kuongoza kabla ya kuchezewa rafu mbaya na beki wa Japan, Tulio kwenye dakika ya 19 ya mchezo huo uliochezwa nchini Uswizi.

Kuumia kwa Drogba ni pigo kwa Ivory Coast ambayo imepangwa kundi la kifo pamoja na Brazili na Ureno.

Akiongea wakati akiwahishwa hospitali kwa matibabu zaidi, Drogba amesema kwamba ndoto yake ya kung'ara kwenye kombe la dunia imeyeyuka kwani hataweza tena kuiwakilisha nchi yake kama alivyopanga.

Lakini baada ya ushauri wa madaktari na operesheni atakayofanyiwa usiku huu, Drogba amesema kwamba amepata matumaini ya kurudi uwanjani kuiwakilisha nchi yake kwenye kombe la dunia ila hajui kama atamudu kulisakata kabumbu vizuri.

Akiongelea hali ya Drogba, kocha wa Ivory Coast Sven-Goran Eriksson amesema kuwa hali halisi ya Drogba itajulikana kesho baada ya ripoti ya madaktari

BWANA CHUCHU AFARIKI DUNIA


Bwana chuchu na kingwendu


Bwana chuchu kushoto.

Aliyekuwa mmiliki wa Band ya chuchu sound,Mkurugenzi wa chuchu radio Yusuph Chuchu na Heratbeat records vilivyopo Zanzibar, amefariki dunia jana jijini Nairobi, mazishi yanafanyika leo visiwani Zanzibar. R.I.P Babu chuchu!!

Yussuf Ahmed Alley alijipatia umaarufu mkubwa miaka ya mwanzoni mwa 2000 na bendi yake ya Chuchu Sound,iliyokua na wakali kama Mao Santiago,Omary Mkali,Waziri Sonyo,marehemu Gabby Katanga na wengine kibao,hasa na kibwagizo cha ''EEH..KWAHERI'' kwenye miondoko ya mduara.

Haijajulikana mara moja chanzo cha kifo chake.Msiba upo Kisima Majongoo na Mazishi yanafanyika kwenye makaburi ya MwanaKwerekwe leo saa 10,kisiwani Zanzibar.

Ina lil laahi wa inna ilayhi rajjoun.......................!!!!