Rais Jakaya kikwete leo anafanya ziara kwa mara nyingine tena mkoani kilimanjaro, ambapo atazindua tawi jipya la benki ya biashara la Kenya –KBC,lililopo mjini moshi.
Hamjambo wananchi wa kilimanjarooooooo!!!!Kwa mujibu wa taarifa ya mkoa wa Kilimanjaro, kesho atafungua mkutano wa mameya wa jiji, miji, wenyeviti na wakurugenzi wa halmashauri za wilaya, utakaofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha polisi mjini moshi.
Rais Kikwete (Katikati) ndani ya vazi la chama tawala na ishara ya chama(kidole gumba).Katika ziara hii, Raisi anatarajiwa kufungua ofisi mpya za makao makuu ya jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro na baadae kuutembelea mradi wa kusambaza maji wa himo, sanjari na kugawa kadi kwa wanachama wapya wa CCM.
Hii ni bendera ya tanzania, nimeonyesha uzalendo kidogo.Leo ni siku ambayo kila mtanzania mpenda soka na yule ambaye hapendi atakuwa makini kusikia matokeo ya mechi ambayo itachezwa usiku kati ya brazil. na taifa stars.Mungu ibariki Taifa stars. Ameni!!!!!!!!!!!!!!!!!
Maeneo ya wazi katika kata ya pasua yamekuwa dampo baada ya kukosa sehemu maalumu ya kuweka taka wakati mpango wa ukusanyaji taka ukipingwa na wananchi.Katika maeneo ambayo manispaa iliweka mankotena imekuwa ikilalamikiwa na wananchi haswa kutokuwepo kwa mankotena hayo na mengine kutoondolewa pindi yanapojaa takataka.Moja kati ya eneo katika kata ya pasua ni eneo la wazi katika mtaa wa majengo mapya ambalo kwa sasa limekuwa eneo la kutupa taka na kuwa hatari ya milipuko ya magojwa. Eneo hili limenzungukwa na nyumba kitu ambacho ni hatari haswa kwa watoto wanaopenda kucheza eneo hilo
Hili ndio eneo la wazi la mtaa wa majengo mapya ambalo limekuwa sehemu ya kutupia taka (jalala).Hii ni changamoto kwa viongozi husika kupambana na hali hii kuepuka na magojwa ya milipuko na maeneo haya ya wazi kubaki na kazi ambayo ndio lengo lake.Think about it!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!